KAMATI ya Mashindano ya Shirikisho la Soka nchini (TFF) ilitangaza ratiba ya hatua ya 16 bora ya michuano ya Azam Sports Federation Cup (ASFC) maarufu kama FA.
Simba ina kazi ya kusaka ushindi dhidi ya African Sports ya Tanga, Machi 2, Uwanja wa Mkapa, Yanga dhidi ya Tanzania Prisons Machi 3 Uwanja wa Mkapa.
Geita Gold watamenyana dhidi ya Green Warriors, Machi 3, Uwanja wa Nyankumbu, Geita, Machi 4, Ihefu Uwanja wa Highland Estates dhidi ya Pan African, Mtibwa Sugar dhidi ya KMC huku Singida Big Stars watamenyana na JKT Tanzania.
Azam FC wataikaribisha Mapinduzi FC Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Machi 5, mwaka huu huku Kagera Sugar wakimenyana na Mbeya City kwenye Uwanja wa Kaitaba.
Hii ni michezo ya 16 bora, ambapo timu nane ambazo zitafanikiwa kushinda kwenye mechi zake itatinga hadi hatua ya robo fainali.
Yanga ndiyo mabingwa watatezi wa kombe hilo, wakilitwaa msimu uliopita mbele ya Coastal Union ambao walitolewa na Simba kwenye hatua ya 32 kufungwa kwenye mchezo wa fainali.