SIMBA YAIVUTIA KASI SINGIDA BIG STARS

BAADA ya kumalizana na Coastal Union kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho kituo kinachofuata kwa Simba ni dhidi ya Singida ig Stars.

Leo Februari Mosi 2023 kikosi cha Simba kimefanya mazoezi kwa ajili ya kuelekea kwenye mchezo huo unaotarajiwa kuchezwa Ijumaa.

Februari 3 utakuwa ni mchezo wa kwanza kwa Simba ndani ya mwezi mpya 2023 baada ya kukamilisha Januari iliyokuwa na mambo mengi kwelikweli.

Roberto Oliveira, Kocha Mkuu wa Simba amesema kuwa wana amini watafanya vizuri kwenye mchezo huo.

Ofisa Habari wa Singida Big Stars, Hussein Masanza amesema kuwa wanahitaji nao pointi tatu.

Mchezo wao wa mzunguko wa kwanza ubao ulisoma Singida Big Stars 1-1 Simba, Uwanja wa Liti na kuwafanya wababe hao kugawana pointi mojamoja.

Hello Februari, Happy New Year 2023.