AZAM FC YAPOTEZA MCHEZO WA KIMATAIFA

KWENYE mchezo wao wa kimataifa dhidi ya Al Hilal uliochezwa Januari 31, timu hiyo ilipoteza mchezo wake.

Baada ya dakika 90 ubao wa Uwanja wa Azam Complex ulisoma Azam FC 0-1 Al Hilal.

Bao pekee la ushindi kwa Al Hilal lilipachikwa dakika ya 45 kupitia kwa Mohamed Abdelrahman ambalo lilidumu mpaka mwisho wa mchezo.

Huo ulikuwa ni mchezo wa kimataifa wa kirafiki ikiwa ni kwa ajili ya maandalizi ya mechi zao za ligi pamoja na Al Hilal kujipanga kwenye mechi za kimataifa.

Azam FC mchezo wake ujao dhidi ya Dodoma Jiji ambao unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Jamhuri,Dodoma.