KLABU ya Singida Big Stars kwa sasa ipo Dara kwa ajili ya maandalizi ya mechi yao ya Ligi Kuu Bara dhidi ya Simba.
Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa, Ijumaa ikiwa ni mzunguko wa pili baada ya ule wa mzunguko wa kwanza kugawana pointi mojamoja kwa kufungana bao 1-1.
Ni nyota Kaseke anayetumikia adhabu ya kufungiwa kucheza mechi tatu mfululizo hatakuwa kwenye mchezo huo na hayupo kwenye kikosi ambacho kipo Dar kwa mujibu wa uongozi wa Singida Big Stars.
Mechi tatu anazozikosa Kaseke ni dhidi ya SBS vs Ruvu Shooting huu ulikuwa ni wa Kombe la Shirikisho ambapo Ruvu Shooting ilipoteza kwa kufungwa mabao 2-1.
Mchezo ujao ni dhidi ya Simba unaotarajiwa kuchezwa februari 3,2023 Uwanja wa Mkapa.
Kigongo cha tatu ni dhidi ya Ihefu itakuwa Februari 12 ambapo itakuwa ugenini.
Sababu kubwa za Kaseke kukosekana kwenye mechi hizo ni kile kilichoelezwa kuwa ni kuonekana akifanya kitendo ambacho kilionyesha masuala ya ushirikina kwenye mchezo dhidi ya Azam FC ubao uliposoma Singida Big Stars 1-0 Azam FC.