UCHAGUZI UMEGOTA MWISHO, MAKUNDI YASIWEPO

Murtaza Mangungu ameshinda uchaguzi nafasi ya Mwenyekiti wa Klabu kwa kupata kura 1,311.

Tayari kwa sasa uongozi mpya umepatikana na kampeni muda wake umekwisha.

Yale yote ambayo ymaetokea kwenye masuala ya uchaguzi pamoja na kampeni ni muhimu kuyafanyia kazi ili kuwa imara wakati ujao.

Kwa walioshinda hongereni na tunatambua kwamba mmetoa ahadi kwa wachama na mashabiki wa Simba.

Wale ambao mmekwama kushinda haina maana hamna uwezo wa kuongoza hapana ni matokeo yameamua iwe hivyo.

Yote kwa yote kazi inabidi iwe moja kwa sasa kuijenga Simba kwa maendeleo ya Tanzania kwenye ulimwengu wa soka.

Zile porojo ambazo mlitoa kwenye kampeni ni muda wake wa kuzifanyia kazi ili kupata matokeo mazuri kwenye utendaji.

Kila kitu kinawezekana na muda ni sasa kufanya kazi yale ambayo mliahidi na mashabiki mzidi kuwa pamoja nao bega kwa bega.

Makundi mwisho ni muhimu kufanya yote kwa ushirikiano mkubwa.