Murtaza Mangungu ameshinda kiti cha Uenyekiti wa klabu ya Simba kwa mara nyingine tena akimpiga chini mgombea Mwenza Moses Kaluwa kwa tofauti ya kura 266.
Katika uchaguzi mkuu wa klabu hiyo uliofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) kuanzia jana Januari 29 hadi lao Januari 30, 2023 Mangungu alipata kura 1311 na Kaluwa kura 1045 katika jumla ya kura halali 2356 huku kura 7 zikiharibika.
Walioshinda nafasi ya wajumbe watano wa Bodi ya Wakurugenzi wa Klabu ya Simba katika uchaguzi uliofanyika jana Januari 29 na kumalizika leo Januari 30, 2023 ni pamoja na :-
Dkt. Seif Ramadhan Muba – kura 1636
Asha Baraka – kura 1564
CPA Issa Masoud Iddi – kura 1285
Rodney Chiduo – kura 1267
Seleman Harubu – kura 1250
Uchaguzi huo ulifanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC), Dar es Salaam.