MABINGWA watetezi wa Kombe la Shirikisho Yanga chini ya Kocha Mkuu Nasreddine Nabi leo Januari 29,2023 wana kazi ya kusaka ushindi kwenye mchezo wa raundi ya tatu.
Yanga inatarajiwa kumenyana na Rhino Rangers FC ambao nao wameweka wazi kuwa wanahitaji ushindi ili kutinga raundi ya 16 bora.
Tayari wapinzani wao wakubwa ambao ni Simba, Singida Big Stars, Azam FC, Mtibwa Sugar na KMC wamekata tiketi ya kutinga hatua ya 16 bora baada ya kushinda mechi zao.
Kwenye mchezo wa leo kuwana mastaa wa Yanga ikiwa ni pamoja na Farid Mussa, Aziz KI, Bernard Morrison na Fiston Mayele VIP A ni 15,000, VIP B na C ni 10,000 na mzunguko ni 5,000.