LEO Jumapili Klabu ya Sima inatarajiwa kufanya mkutano mkuu wenye ajenda 13 ikiwemo suala la uchaguzimkuu wa kuchagua mwenyekiti na wajumbe watano wa Bodi ya Wakurugenzi.
Katika uchaguzi huo wanaowania nafasi ya mwenyekiti ni Murtanza Mangungu anayetetea kiti chake na Moses Kaluwa.
Wajumbe ni Seif Ramadhan Muba, Seleman Harub Said,Iddi Halifa Kitete,Issa Masoud Iddi,Abubabakar Zebo,Abdallah Rashid Mgomba, Elisony Edward Mweladzi, Rashid Mashaka Khamsini,Rodney Makamba Chiduo,Aziz Mohamed, Asha Baraka na Pendo Aidan Mapugilo.
Mkutano huo unatarajiwa kufanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere, (JNICC) Dar, kuanzia saa 2 asubuhi.
Mkutano huo umekuwa ukifanyika kuangalia maendeleo ya klabu huku safari hii ukiambatana na uchaguzi mkuu ambao wenyewe hufanyika kila baada ya miaka minne.
Mangungu anayemaliza muda wake aakibarua cha kupambana na Kaluwa anayeitaka nafasi hiyo.