HAKUNA anayependa kuona anakosa nafasi ya kuanza kikosi cha kwanza kwenye mechi ambazo timu yake itakuwa inacheza ndani ya uwanja.
Imekuwa kawaida kwa wachezaji wanaopewa nafasi kutoonyesha utofauti wao na yule ambaye anakuwa asungua benchi jambo ambalo linapaswa kuwa tofauti.
Sababu kubwa ya wachezaji kuwekwa benchi ni kushindwa kwenda na mpango kazi wa benchi la ufundi na wakati mwingine huwa inakuwa mbinu kwa ajili ya kubadilisha matokeo ila imekuwa tofauti.
Wale ambao mzunguko wa kwanza walipewa nafasi wakashindwa kuzitumia muda wa kukamilisha na kufanya mabadiliko ni sasa kwa kuwa hakuna muda wa kupoteza.
Kwa sasa kila kocha anahitaji mchezaji ambaye atampa matokeo ya ushindi na sio mchezaji wa kufanya majaribio ndani ya uwanja.
Ikiwa ulifanya vibaya mzunguko wa kwanza na bado hujajirekebisha mzunguko wa pili hata benchi unaweza usikae na badala yake ukawa jukwaani kabisa.
Hapa ni mwendo wa lala salama yule mwenye juhudi kwenye kila mechi anapewa kipaumbele kwenye mechi za ligi pamoja na mashindano mengine.
Wapo ambao wameanza kwa kusuasua ni muda wao kufanya mabadiliko na kuamua kujituma bila kuogopa.
Vipaji walivyonavyo ni dhahabu lazima vipitishwe kwenye moto ili kuongeza thamani kama watajionea huruma muda wao wa kujutia unakuja.
Hakika ligi ina ushindani mkubwa na kila mmoja anahitaji kuonyesha uwezo wake basi ikawe hivyo kwenye mzunguko wa pili.