WAKALI WA KUTUPIA HAT TRICK, KAFUNGUA 2023

MASTAA wanne ndani ya Ligi Kuu Bara wametupia hat trick ndani ya Ligi Kuu Bara msimu wa 2022/23.

Nyota wa kwanza kufanya hivyo ni Fiston Mayele wa Yanga ambaye alifunga mbele ya Singida Big Stars.

Ni Novemba 17,2022 ubao wa Uwanja wa Mkapa ulisoma Yanga 4-1Singida Big Stars ambapo bao la Singida Big Stars lilipachikwa na Meddie Kagere aliyemtungua Aboutwalib Mshery.

John Bocco alifunga mbele ya Ruvu Shooting Novemba 19,2022 Simba ilishinda mabao 4-0 Uwanja wa Mkapa lile lingine la Simba lilifungwa na Shomary Kapombe.

Mchezo mwigine Bocco alifunga hat trick mbele ya Tanzania Prisons Uwanja wa Mkapa ubao uliposoma Simba 7-1 Prisons na Said Ntibanzokiza naye mchezo huo ukiwa ni wa kwanza kwake alifunga hat trick lile lingine moja ni mali ya Kapombe.

Mwamba mwingine ambaye amefungua 2023 kwa kufunga hat trick ni Ibrahim Mukoko nyota wa Namungo FC aliyemtungua mabao yote David Kissu, Uwanja wa Uhuru.

Ubao ulisoma KMC 1-3 Namungo na mwamba akasepa na mpira wake jumlajumla.