NI imani Kajula ametangazwa kuwa Mtendaji Mkuu mpya wa Simba SC akichukua nafasi ya Barbra Gonzalez ambaye alitangaza kujiuzulu kwenye nafasi hiyo.
Mtendaji huyo mpya ameweka wazi kuwa anafurahi kujiunga na timu hiyo kwenye nafasi hiyo.
Aidha amesema yeye ni shabiki na mwanachama wa timu hiyo kwa muda mrefu.
“Mimi ni shabiki kindakindaki wa Simba na ni mwanachama pia wa Simba kwa hapa nimefurahi kupata nafasi hii.
“Nimependa kujiunga na Simba kwa nafasi hii nina amini wamba nitafanya kazi kwa ushirikiano na wenzangu kwa ajili ya kufikia mafanikio na inawezekana,”