MANGUNGU AZUNGUMZIA USHIRIKIANO NA MIPANGO KAZI

MURTANZA Mangungu, Mwenyekiti wa Simba ambaye anatetea kiti hicho kwa mara nyingine amesema kuwa hata kama akishindwa atabaki kushirikiana na Simba kwa kuwa ni mwanachama wa timu hiyo.

Januari 29,2023 Simba wanatarajia kufanya uchaguzi na mkutano mkuu ambapo kwa sasa kampeni zinaendelea.

Mangungu amesema kuwa anatambua kwenye ushindani kuna kushinda na kushindwa lakini yeye hana tatizo.

“Ambacho ninaweza kuwaambia wanachama wa Simba wanipe kura kwa kuwa ninauzoefu na kwa kushirikiana tutafanya kazi kubwa.

“Kura zao ni muhimu ili kufikia malengo ambayo tunayo inawezekana kutokana na kila mmoja kuhitaji kuona tunafikia malengo yetu kitaifa na kimataifa,”amesema Mangungu.