SAKATA LA FEI TOTO NGOMA NZITO

FEI Toto nyota wa Yanga inatajwa kuwa ameongeza mwanasheria mwingine kwenye sakata ya kesi yake na Yanga.

Kiungo huyo amemuongeza mwanasheria huyo baada ya kuomba, ‘review’ juu ya majibu ya kesi yake.

Tayari majibu kuhusu sakata lake awali yalitolewa na Kamati Tendaji ya Shirikisho la Soka Tanzania, (TFF) kuhusiana na shauri lake ambalo liliwasilishwa na Klabu ya Yanga kuhusu kuvunja mkataba kwa nyota huyo.

Yanga walifungua shauri hilo wakipinga maamuzi ya kiungo huyo ya kuvunja mkataba na kurejesha 112 Milioni ambacho alitoa kwa ajili ya kuvunja mkataba.