YANGA YAIVUTIA KASI RUVU SHOOTING

ALI Kamwe, Ofisa Habari wa Yanga ameweka wazi kuwa wapo tayari kwa ajili ya mchezo wao wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Ruvu Shooting.

Mchezo huo awali ulitarajiwa kuchezwa Januari 21 lakini umepelekwa mbele mpaka Januari 23,2023 Uwanja wa Mkapa.

Kamwe amebainisha kuwa wanatambua mchezo huo utakuwa mgumu lakini wapo tayari kupata ushindi.

“Moja ya mchezo mgumu ambao utakuwa na ushindani mkubwa lakini tupo tayari na wachezaji wanajua kwamba ambacho kinahitajika ni pointi tatu.

“Kila mchezo kwetu ni mgumu hivyo nasi tunafanya maandalizi mazuri ili kupata ushindi ambayo ni furaha kwetu na mashabiki kiujumla,” amesema.

Mchezo wao wa fungua mwaka 2023 Yanga yenye pointi 53 ikiwa namba moja iliwatungua Ihefu bao moja huku mtupiaji akiwa ni Fiston Mayele.

Ruvu Shooting kwenye msimamo ipo nafasi ya 15 ina pointi 14 baada ya kucheza mechi 20.