LILE PIRA DUBAI LA SAMBA LOKETO LILIPIGWA NA NYUNDO

ILIKUWA mwendo wa msako wa pointi tatu kwa timu zote mbili ambazo msimu wa 2022/23 zimekuwa zikionyeshana ubabe haswa ndani ya dakika 90.

Simba inayonolewa na Kocha Mkuu, Roberto Oliviera iliyotamba kuja na pira Samba Loketo liligongwa nyundo kinomanoma na Mbeya City inayonolewa na Adallah Mubinu.

Mchezo wa fungua mwaka 2023 kwa Simba na mchezo wa kwanza kwa Oliviera kukaa benchi.

Hapa tunakuletea namna pira lilivyopigwa na kazi kwa baadhi ya wachezaji wa timu zote mbili namna hii:-

Air Manula kwenye balaa

Aishi Manula kipa namba moja wa Simba  alikutana na balaa zito baada ya kutunguliwa mabao mawili na wachezaji wa Mbeya City.

Unakuwa ni mchezo wa pili kwa Manula kutunguliwa mabao mawili kwenye ligi akiwa Uwanja wa Mkapa ule wa kwanza alitunguliwa na KMC na wa pili ni dhidi ya Mbeya City.

Weka kando bao la kwanza alilotunguliwa na Richardson Ng’odya dakika ya 13 litazame bao la pili alilotunguliwa na Juma Shemvuni ambaye hakuwa na mpango wa kufunga akiwa nje ya 18 kwa pigo la faulo ndefu iliyoonekana kutokuwa na hatari kwa Manula.

Manula alikuwa ametoka nje ya eneo lake katika jitihada za kurejea kuokoa hatari hiyo alishuhudia mpira ukijaa nyavuni na kuishia kuambulia kadi ya njano baada ya kumchezea faulo Tariq Seif.

Kapombe

Shomary Kapombe mzee wa kumwaga maji pira Dubai lilibuma kwake krosi zake hazikuleta matunda na miongoni mwa krosi aliyopiga ilikuwa dakika ya 20, aliishia kucheza faulo dakika ya 19,54 alipiga shuti lililoenga lango dakika ya 37.

Zimbwe

Ni yeye alisababisha penalti ya Simba dakika 45 na mwamuzi wa kati Ester Albert kuamua liwe tuta lilifungwa na Saidi Ntibanzokiza ilikuwa dakika ya 48.

Huyohuyo Mohamed Hussein Zimbwe Jr alicheza faulo iliyoleta bao kwa Mbeya City ilikuwa dakika ya 77 alipomcheza Salum Kihimbwa na ilipigwa na Juma Shemvuni aliyemtungua Manula dakika ya 78.

Alipiga shuti ambalo halikulenga lango dakika ya 37, alichezewa faulo dakika ya 45 na 86.

Onyango na Outtara

Joash Onyango alicheza faulo dakika ya 61,64 ambapo alionyeshwa kadi moja ya njano aliokoa hatari dakika ya 62,64,89 na 90 kwenye ulinzi alianza na Mohamed Outtara aliyeokoa hatari dakika ya 57.

Sadio

Sadio Kanoute mzee wa kutembeza mikato alifanya hivyo dakika ya 9,18 na 42 alipoonyeshwa kadi ya njano.

Chama na Pape

Clatous Chama alitoa pasi ya bao dakika ya 10 kwa Saidi Ntibanzokiza alicheza faulo dakika ya pili na alitumia dakika 33 nafasi yake ilichukuliwa na Pape Sakho aliyefunga bao dakika ya 55 alionyeshwa kadi ya njano dakika ya 90 aliotea dakika ya 74 na 75.

Bocco na Kibu

John Bocco aliyeyusha dakika 33, aliotea dakika ya 21 nafasi yake ilichukuliwa na Kibu Dennis aliyepiga nje ya lango mashuti dakika ya 73,89 alichezewa faulo dakika ya 60 na 90.

Kyomo

Habib Kyombo utulivu ulikuwa mdogo alikosa nafasi ya wazi kufunga dakika ya 83 aliotea dakika ya 17 na 52 alicheza faulo dakika ya 2 na 45 alipiga mashuti yaliyolenga lango dakika ya 28 na 71.

Mzamiru

Mzamiru Yassin jasho lilimvuja dakika 90 alicheza faulo dakika ya 23,49 na 56 alionyeshwa kadi ya njano.

Ntibanzokiza

Alipachika mabao mawili dakika ya 10 na 48 kwa mkwaju wa penalti, alicheza faulo dakika ya 74 na 90.

Mbeya City walionyesha kwamba hata Bongo kuna kambi matata ambapo walipiga kazi namna hii:-

Lameck Kanyonga aliokoa hatari dakika ya 28 na 37 alitunguliwa dakika ya 10,48 na 55.

Kunambi

Nyota Keneth Kunambi huyu alicheza faulo dakika ya 71 na 90.

Madeleke

Samson Madeleke alionyeshwa kadi nyekundu dakikaya 65 baada ya kuonyeshwa kadi mbili za njano ile ya awali alionyeshwa dakika ya 52.

Juma Shemvuni

Alipewa majukumu ya kupiga faulo pia alifanya hivyo dakika ya 2 na ile ya dakika ya 78 ilimshinda Manula kuokoa ikazama kambani.

Ng’odya

Richardson Ng’odya nyota wa Mbeya City alipachika bao dakika ya 13 alipiga mashuti yaliyolenga lango dakika ya 5,6,24,44 aliotea dakika ya 56.

Nassoro

Hassan Nassoro alionyeshwa kadi ya njano dakika ya 46 alipiga faulo dakika ya 18 na 57

Awadhi Juma

Alipiga mashuti yaliyolenga lango la Manula dakika ya 8 na 9 pia alifanya hivyo.

Kihimbwa

Kutana na mchezaji aliyechezewa faulo nyingi na mastaa wa Simba ikiwa ni pamoja na Kanoute,Zimbwe,Kapombe ilikuwa dakika ya 42,54,56,74,78 alipiga kona dakika ya 81 alikuwa msumbufu mwanzo mwisho.

Makala haya yameandikwa na Dizo Click kutoka Championi