KUPATWA KWA PIRA DUBAI UWANJA WA MKAPA

DAKIKA 90 zilikuwa za kazi huku pira Dubai likionekana kupatwa tabu mbele ya Mbeya City ambao walionesha ushindani wakitaka kusepa na pointi.

Dakika tatu ziliwatosha Mbeya City kusawazisha bao la Ntibanzokiza dakika ya 10 kupitia kwa Richardson Ngo’dya ambaye alitumia makosa ya mabeki wa Simba.

Kipindi cha pili Simba ilipata bao lililoonekana kulalamikiwa na wachezaji kutokana na mazingira ya penalti iliyosababishwa na Zimbwe mtupiaji akiwa ni Ntibanzokiza.

Bao la tatu kwa Simba lilifungwa na Pape Sakho aliyechukua nafasi ya Clatous Chama alipachika bao hilo dakika ya 55.

Aishi Manula kwenye siku mbaya kazini, kiwango chake kikiwa kwenye misukosuko alijifunga bao dakika 78 kwenye harakati za kuoko hatari ya Mbeya City ambao walikuwa pungufu baada ya mchezaji wao mmoja kuonyeshwa kadi nyekundu.

Huu ni mchezo wa kwanza kwa Robert Oliviera raia wa Brazil kukaa benchi kwenye mechi za ligi.