UBAO wa Uwanja wa Mkapa umesoma Yanga 1-0 Ihefu ikiwa ni mchezo wa Ligi Kuu Bara.
Ihefu watajilaumu wenyewe kwa kutunguliwa kwenye mchezo wa leo kutokana na makosa ambayo wameyafanya kipindi cha pili.
Shukrani kwa Fiston Mayele ambaye alipachika bao pekee la ushindi dakika ya 63 akitumia makosa ya kipa wa Ihefu Fikirini Bakari kwenye muda wa kuanzisha mashambulizi.
Jitihada za mabeki wa Ihefu kuokoa hatari hiyo wakiongozwa na legend Juma Nyoso hazikuzaa matunda na kuruhusu bao la kwanza na la ushindi kwa Yanga.
Kenned Musonda ambaye amekabidhiwa jezi na 25 alipata nafasi ya kuingia kipindi cha pili kwenye mchezo huo wa usiku wa kisasi.
Sasa Yanga ambao walipoteza mbele ya Ihefu kwa kufungwa mabao 2-1 wamelipa kisasi kwa bao moja na kusepa na pointi tatu