Skip to content
KAZI kubwa kwa sasa kwa timu zote ambazo zinashiriki Ligi Kuu Bara, Championship na Ligi ya Wanawake ni kusaka ushindi.
Ipo wazi baada ya mapumziko ya muda kutokana na ratiba mbalimbali tayari mambo yanaanza kurejea taratibu.
Tunaona wale ambao walikuwa kwenye Kombe l Mapinduzi wamerejea na waliokuwa wakifuatilia wameshuhudia bingwa mpya.
Hongera kwa Mlandege kwa kufanya kazi kubwa kwenye kusaka ushindi nah ii inaonyesha kwamba kwenye soka kila kitu kinawezekana.
Matokeo ya dakika 90 umuhimu wake mkubwa ni kuonyesha kitu ambacho wengi walikuwa hawatarajii lakini kinatokea.
Kwa maana hiyo hata kwa zile timu ambazo zimekuwa kwenye kupambana kujinasua kutoka kwenye hatua ya kushuka daraja zina muda wa kufanya vizuri.
Labda wachezaji wanaweza kuamini kwamba wana mechi mkononi lakini muda hausubiri kwani kila siku kunakuwa na tofauti.
Ambacho kinatakiwa kwa sasa ni kila timu kufunga mkanda na kupambana kupata matokeo chanya kwenye mechi ambazo wanacheza.
Kila la kheri kwenye maandalizi katika mechi za mzunguko wa pili lakini msisahau kwamba kuna suala la kushuka daraja.