KIPA Metacha Mnata ambaye ni kipa mzawa atkuwa ndani ya kikosi cha Yanga kinachopambana kutetea taji la ligi.
Kipa huyo aliwahi kuitumikia Yanga kabla ya kukamilisha mkataba wake na kuachana naye kisha nafasi yake akaichukua Eric Johora.
Johora hakuwa na mwendo mzuri ndani ya kikosi cha Yanga kwa kuwa hakuwa na uhakika wa kuanza kikosi cha kwanza cha Yanga na badala yake alikuwa ni kipa namba tatu.
Kipa namba moja ni Djigui Diarra namba mbili ni Aboutwalib Mshery ambaye huyu ni mzawa.
Miongoni mwa timu ambazo Mnata amecheza ni pamoja na Mbao FC, Singida Big Stars, Polisi Tanzania na sasa anakuwa ndani ya kikosi cha Yanga.
Anakuwa nyota wa nne kutambulishwa ndani ya kikosi cha Yanga baada ya Mudathir Yahya, Mamdou Doumbia na Musonda ambaye ni mshambuliaji.
Ni kwa mkopo wa miezi sita anajiunga na kikosi cha Yanga.
Mnata alikuwa kwenye kikosi cha fainali ya Kombe la Mapinduzi dhidi ya Mlandege FC ambapo Singida ilipoteza kwa kufungwa mabao 2-1 dhidi ya Mlandege na kugotea kuwa nafasi ya pili 2023.