Morocco imejiondoa katika kutetea taji lao la Ubingwa wa Mataifa ya Afrika (CHAN) mwezi huu baada ya kukataliwa kusafiri moja kwa moja hadi taifa mwenyeji Algeria.
Uhusiano wa kidiplomasia kati ya majirani hao wa kaskazini mwa Afrika ulikatishwa na Algeria mnamo 2021, na kwa hatua hiyo, safari zote za ndege za moja kwa moja kati ya nchi hizo mbili zilisitishwa.
Shirikisho la Soka la Morocco (FMRF) lilisema mnamo Desemba hawatahudhuria isipokuwa wakiruhusiwa kusafiri moja kwa moja kutoka mji mkuu wao, Rabat, ndani ya shirika la ndege la taifa la nchi hiyo, Royal Air Maroc (RAM).
Michuano hiyo ambayo Atlas Lions ilishinda mwaka wa 2018 na 2020 , itaanza Ijumaa kwa Algeria kuwakaribisha Libya na ni michuano ya kimataifa ya Shirikisho la Soka Afrika (Caf) kwa wachezaji wanaocheza ligi za ndani katika bara hilo.
Morocco ilikuwa ianze kuwinda taji la tatu mfululizo Jumapili dhidi ya Sudan, lakini FMRF ilisema katika taarifa yake: “(Sisi) tuliarifiwa Desemba 22 na Caf kwamba idhini kimsingi imepatikana. Kupatikana kwa idhini ya mwisho. kwa bahati mbaya haijathibitishwa na Caf.
“FRMF imewasilisha maelezo ya mpango wa ndege na kuratibu ili kupata idhini ya mwisho ya safari ya RAM kutoka Rabat na kuendelea na maandalizi ya safari na ushiriki katika CHAN.”
BBC imeitaka CAF kuthibitisha kwamba vikwazo ni tu kupigwa marufuku kutoka CHAN 2024 – na kwa hivyo haimaanishi kwamba washindi wa nusu fainali ya Kombe la Dunia watazuiwa kushiriki mashindano yote ya Caf, pamoja na Kombe la Mataifa ya Afrika linalofanyika Ivory Coast mwaka ujao.
Morocco ilicheza mechi mbili za kirafiki dhidi ya Ethiopia kwenye kambi yao ya mazoezi huko Salé wiki hii kabla ya safari ya ndege ambayo walitarajia kupanda moja kwa moja hadi Constantine, ambapo wangewekwa kwa ajili ya mashindano hayo.