ABDUL Suleiman, ‘Sopu’ kiungo mshambuliaji wa Azam FC amesema ushindi ambao wameupata mbele ya Jamhuri ni zawadi kwa mashabiki.
Januari 5,2023 Azam FC ilipata ushindi wake kwenye mchezo wa Kombe la Mapinduzi dhidi ya Jamhuri.
Sopu kwenye mchezo huo alitupia mabao mawili na kuchaguliwa kuwa nyota wa mchezo huo.
Timu hiyo inatinga hatua inayofuata ya nusu fainali ikiwa imekusanya pointi nne sawa na Malindi tofauti ni idadi ya mabao ya kufunga na kufungwa.
Nyota huyo amesema:”Kwetu kupata ushindi ni furaha na zawadi kwa mashabiki ambao wanaifuatilia timu hiyo kwenye kila mechi.
“Tumefurahi kupata matokeo mazuri na hili ni jambo kubwa kwetu tutazidi kupambana kwenye mechi zijazo kupata matokeo chanya.”.