KOCHA Mkuu wa Yanga, Nasreddine Nabi amewapa maagizo mazito wachezaji wa timu hiyo ikiwa ni pamoja na Fiston Mayele, Aziz KI, Khalid Aucho na Dickson Job wakati huu wa mapumziko.
Nyota hao ni miongoni mwa wale ambao watakosekana kwenye Kombe la Mapinduzi 2023 visiwani Zanzibar.
Meneja wa Yanga,Walter Harrison amesema kuwa wachezaji wote wapo tayari kwa ajili ya Kombe la Mapinduzi.
“Wapo wachezaji hawatashiriki Kombe la Mapinduzi na benchi la ufundi linatambua hivyo kuelekea mashindano haya yenye ushindani tunaamini kwamba tutapa matokeo mazuri.
“Wale ambao hawatakuwa kwenye mashindano katika mapumziko yao wataendelea na mazoezi binafsi kama ambavyo wamepewa na benchi la ufundi,” amesema.
Mchezo wa kwanza wa Yanga kwenye Kombe la Mapinduzi 2023 iliibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya KMKM bao la ushindi likifungwa na Dickosn Ambundo.