MENEJA wa Mawasiliano wa Simba SC, Ahmed Ally amefunguka na kusema kuwa katika dirisha hili dogo la usajili hawana mpango wa kumsajili aliyekua kiungo wa Klabu ya Vipers, Bobosi Byaruhanga.
Akizungumza na Spoti Xtra, Ally alifunguka: ” Tunatarajia kuongea nguvu katika eneo la kiungo mkabaji ambaye atatusaidia kutimiza malengo yetu msimu huu.
“Hatuwezi kumsajili Bobosi kwasababu tayari alishawahi kushiriki michuano ya kimataifa msimu huu, hivyo hatoweza kuwa na mchango wowote katika michuano yetu ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
“Tunahitaji mchezaji ambae tutaweza kumtumia katika michuano au mashindano yote tunayoshiriki ndani na nje ya nchi.
“Kumsajili Bobosi itakua ni kama tumemsajili kwa ajili ya kucheza mechi kumi za Ligi Kuu Bara zilizobaki tu jambo ambalo hatuwezi kufanya.
“Bobosi ni mchezaji kijana mwenye viwango na ubora wa hali ya juu, lakini msimu huu hatuwezi kumsajili.”