BAADA ya kupoteza mchezo wa kwanza wa Kombe la Mapinduzi 2023 mbele ya Kocha wa mpira, Roberto Oliviera kikosi cha Simba kina kazi nyingine ya kusaka ushindi kesho, Uwanja wa Amaan.
Simba imevuliwa ubingwa kwa kutunguliwa bao 1-0 dhidi ya Mlandege kutokana na makosa ya safu ya ulinzi pamoja na ile ya ushambuliaji.
Mpango mzuri wa kuokoa hatari ya pigo la kona dakika ya 75 ulikwama kwa mabeki wa Simba baada ya kumpa nafasi beki Abubakar Mwadin kuwatungua bao la ushindi dakika ya 75.
Ni safu ya ushambuliaji ya Simba inayoongozwa na Kibu Dennis na Habib Kyombo ilikwama kupiga shuti ambalo lililenga lango katika dakika 45 za mwanzo jambo liliwapa matokeo yakupoteza mazima.
Ni mchezo wa mwisho Simba kucheza ambapo haitakuwa na huduma ya nyota wake Clatous Chama mwenye tuzo ya mchezaji bora chaguo la mashabiki Desemba 2022.