PENALTI YAZUA UTATA FUNGUA MWAKA

JANUARI Mosi 2023 ilishuhudiwa penalti ambayo iliwafanya wachezaji wa Namungo FC kuonekana wakimlalamikia mwamuzi kutokana na mazingira ya penalti hiyo kuleta utata.

Langoni kwa Namungo FC alikaa kipa mzawa Deogratius Munish, ‘Dida’ ambaye hakuwa na chaguo kutokana na mpigaji kupiga kwa umakini.

Ni Maabad Maulid alifunga bao hilo akisawazisha bao lililofungwa na Ibrahim Mkoko nakuwafanya wagawane pointi mojamoja.

Ubao wa Uwanja wa Coastal Union ulisoma Coastal Union 1-1 Namungo.

Leo Januari 3, 2023 kikosi cha Namungo kimeanza safari kuelekea Zanzibar kwa ajili ya kushiriki Kombe la Heshima la Mapinduzi Cup 2023.