MUDHATHIR Yahaya kiungo wa zamani wa Azam FC ametambulishwa ndani ya Yanga leo Januari 3,2023 ikiwa ni usajili wa kwanza kwa Yanga dirisha dogo.
Muda kapewa dili la miaka miwili kwa ajili ya kuitumikia timu hiyo inayonolewa na Nasreddine Nabi.
Ikumbukwe kwamba awali nyota huyo alikuwa anatajwa kuwa kwenye rada za Simba ambao wanatajwa kufanya naye mazungumzo.
Nyota huyo anaibuka ndani ya Yanga akiwa ni mchezaji huru baada ya kuachana na mabosi wake wa zamani Azam FC