>

SIMBA KUIBUKIA ZANZIBAR

MABINGWA watetezi wa Kombe la Mapinduzi Simba leo Januari 2,2023 wanatarajiwa kuanza safari kuelekea Zanzibar.

Chini ya Kocha Mkuu mzawa Juma Mgunda kikosi hicho kinaelekea kuanza safari ya kutetea taji lao pekee ambalo walitwaa 2022.

Ikumbukwe kwamba Simba ilishinda bao 1-0 dhidi ya Azam FC kwenye mchezo uliokuwa na ushindani mkubwa na bao pekee la ushindi lilifungwa na Meddie Kagere.

Kagere kwa sasa yupo kwenye changamoto mpya na Singida Big Stars ambao nao pia watashiriki kuwania taji hilo la heshima.

Ahmed Ally, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba amesema kuwa wanakwenda kufanya kazi kubwa kwenye Kombe la Mapinduzi ili warejee wakiwa bora.

“Januari tunaanza na Kombe la Mapinduzi kisha tukirudi kazi inaendelea kwenye ligi na mashindano ya kimataifa mashabiki wazidi kuwa pamoja nasi,”.

Mchezo wa kwanza Simba ni Januari 3,2023 dhidi ya Mlandege.