MSHAMBULIAJI YANGA NI COASTAL UNION

MSHAMBULIAJI Yusuph Athuman ambaye ni mali ya Yanga kwenye mzunguko wa pili atakuwa ndani ya kikosi cha Coastal Union.

Coastal Union wamemchukua nyota huyo kwa mkopo ili kuongeza nguvu kwenye eneo la ushambuliaji.

Hakuwa na nafasi kikosi cha kwanza cha Yanga kutokana na ushindani wa namba ambapo ni Fiston Mayele alikuwa akianza kikosi cha kwanza.