BAADA ya kumaliza mchezo wa funga mwaka dhidi ya Mtibwa Sugar nyota Fiston Mayele ni miongoni mwa wale ambao wamepewamapumziko.
Katika msafara wa leo wa kikosi cha Yanga ulioelekea Zanzibar, Mayele hakuwa kwenye kikosi hicho.
Nyota wengine ni Aziz KI, Kibwana Shomari, Khalid Aucho, Yannick Bangala ambapo wote hawa wamepewa mapumziko.
Kwa mujibu wa meneja wa kikosi cha Yanga, Walter Harrison amesema kuwa sababu ya kuwatumia vijana kwenye Kombe la Mapinduzi Cup ni kuwapa uzoefu pamoja na uwezo ambao wanao.
“Wachezaji wote wana uwezo na tumechanganya wachezaji wa timu kubwa pamoja na ile ya vijana lengo ni kuona wanapata uzoefu na kuleta ushindani,”
Ni Januari 4 Yanga itakuwa na mchezo wake wa kwanza katika Mapinduzi dhidi ya KMKM.