MABAO 11 ya Simba leo yanatarajiwa kukosekana uwanjani kutokana na matatizo ya wachezaji hao.
Ni Moses Phiri ambaye ni mshambuliaji namba moja akiwa ametupia mabao 10 na Peter Banda yeye ametupia bao moja.
Mastaa hawa wote hawatakuwa kwenye mchezo wa leo dhidi ya KMC kwa kuwa hawapo fiti jambo litakalowafanya wakosakane kwenye mchezo huo.
Ikumbukwe kwamba kwenye mchezo wa kwanza uliochezwa Uwanja wa Mkapa ubao ulisoma Simba 2-2 KMC hivyo leo mchezo huo unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa.
Ahmed Ally, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba amesema kuwa Phiri yupo kwenye matibabu ambapo atarejea uwanjani hivi karibuni.