IHEFU HAWANA JAMBO DOGO WATOA ZAWADI YA CHRISTMAS

KABLA ya mabox kuanza kufunguliwa tayari Ihefu wameshakamilisha kutoa zawadi yao kwa mashabiki zao.

Ni msimu wa sikukuu wa Christmas na Mwaka Mpya 2023 pointi tatu waliziweka kibindoni na kuwapa zawadi ya furaha mashabiki zao.

Baada ya dakika 90 ubao wa Uwanja wa Highland Estate, Septemba 24 ulisoma Ihefu 3-1 Mtibwa Sugar.

Mabao kwenye mchezo huo ambao dakika 45 za mwanzo milango ilikuwa migumu yalifungwa na Ismail Mhesa dakika ya 52 kwa Mtibwa Sugar.

Joseph Mahundi alitupia kambani mabao mawili ilikuwa dakika ya 60 na 88 huku bao lingine likifungwa na Orey Chirwa dakika ya 74.

Merry Christmas