FIFA INACHUNGUZA SALT BAE ‘ALIVYOFIKA UWANJANI’ BAADA YA FAINALI

FIFA inachunguza jinsi mpishi maarufu Salt Bae na watu wengine kadhaa walipata “nafasi isiofaa” kufika uwanjani mwishoni mwa fainali ya Kombe la Dunia nchini Qatar.

Salt Bae, mpishi wa Uturuki ambaye jina lake halisi ni Nusret Gokce, alionekana katika picha akiwa ameshika na kubusu kombe la Kombe la Dunia akisherehekea na wachezaji wa Argentina baada ya ushindi wao dhidi ya Ufaransa.
Salt Bae alionekana akibusu Kombe la Dunia

Sheria za Fifa zinasema kombe hilo linaweza tu kushikiliwa na kundi la watu “walioidhinishwa”, wakiwemo washindi wa mashindano, maafisa wa Fifa na wakuu wa nchi.

Baada ya tathmini, Fifa imekuwa ikibaini jinsi watu binafsi walivyoweza kuingia uwanjani baada ya sherehe za kufunga michuano hiyo katika uwanja wa Lusail mnamo Desemba 18.