YANGA KAZI INAENDELEA

VINARA wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Yanga wameweka wazi kuwa mzunguko wa pili utatoa dira ya wao kufanikisha malengo ya kutetea taji hilo.

Timu hiyo imekuwa kwenye mwendo bora wa kupata matokeo licha ya kupoteza mchezo mmoja kati ya 17 ilipotunguliwa na Ihefu mabao 2-1.

Kwa sasa ipo kwenye maandalizi kuelekea kwenye mchezo wao dhidi ya Azam FC unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa Desemba 25.

Cedrick Kaze, kocha msaidizi wa Yanga amesema kuwa kila mchezaji anajua kwamba mzunguko wa pili ni mgumu jambo ambalo linawafanya kupambana bila kuchoka.

Miongoni mwa wachezaji wa Yanga ambao wamekuwa kwenye ubora wao ni pamoja na Jesus Moloko mwenye pasi tatu za mabao na ametupia bao moja, Feisal Salum mwenye, Fiston Mayele ambaye ni kinara wa utupiaji akiwa nayo 13 kwenye ligi.

Kaze amesema:”Mzunguko wa pili una ushindani mkubwa nasi tunafanya maandalizi mazuri kuwakabili wapinzani wetu,”.