NYOTA Vivian Corazone Aquino ambaye alianza kusugua benchi kwenye dabi ya Wanawake limetosha kuipa pointi moja Simba Queens ilikuwa dakika ya 59.
Baada ya dakika 90 kukamilika kwenye mchezo wa leo Desemba 22,2022 ubao wa Uwanja wa Mkapa ulisoma Simba Queens 1-1 Yanga Princess.
Vivian aliweka mzani sawa kipindi cha pili na kufuta bao matata la kichwa kutoka kwa Chioma Wangu dakika ya 45.
Aliachia shuti kali kwa mguu wa kulia akiwa nje ya 18 baada ya kupokea mpira kutoka kwa nyota wa Yanga Princess aliyekuwa akiokoa hatari.
Chioma alifunga bao safi akitumia makosa ya walinzi wa Simba Queens kwenye mpira wa kona uliopigwa zikiwa zimebaki sekundi kadhaa kwenda mapumziko.