BAADA ya kucheza mechi 17, Geita Gold wanafikisha kibindoni jumla ya pointi 23 ndani ya Ligi Kuu Bara.
Kwenye msimamo ipo nafasi ya 7 huku Azam FC ikiwa nafasi ya tatu na kibindoni ina pointi 38 na zote zipo ndani ya 10 bora kweye ligi.
Ndani ya daika 180 kwenye mechi mbili wakiwa nyumbani wamekwama kusepa na pointi zote sita zaidi wameambulia pointi moja.
Pointi hiyo wameipata kwenye mchezo dhidi ya Azam FC uliochezwa Desemba 20 ambapo ubao ulisoma Geita Gold 1-1 Azam FC.
Timu hiyo ndani ya dakika 180 imeokota nyavuni mabao sita ambapo ilitunguliwa mabao matano na Simba kisha bao moja dhidi ya Azam FC.
Geita Gold ipo mikononi mwa mzawa Felix Minziro ambaye ni miongoni mwa makocha wenye uzoefu na uwezo mkubwa kwenye kutimiza majukumu yake.
Kasi yake kwenye dakika 180 katika mechi mbili za mzunguko wa kwanza imekuwa ngumu kutokana na kushindwa kupata matokeo chanya.
Minziro ameweka wazi kuwa makosa watafanyia kazi ili kuwa imara kwa mechi zijazo.