WATANI WA JADI VITANI KUSAKA POINTI TATU

LIGI ya Wanawake Tanzania inaendelea ambapo watani wa jadi wote Simba Queens na Yanga Princess mechi zao za ufunguzi walipasuka.

Kesho Desemba 22 unatarajiwa kuchezwa mchezo wa watani wa jadi wenye rekodi zinazofanana.

Simba Queens wao walinyooshwa mabao 2-1 dhidi ya JKT Queens huku Yanga Princess wao wakinyooshwa bao 1-0 dhidi ya Fountain Gate Princess ambapo baada ya mchezo huo benchi la Yanga lilivunjwa mazima.

Kwa sasa Yanga Princess ipo mikononi mwa Sebastian Nkoma ambaye aliipa ubingwa Simba Queens msimu uliopita kwa sasa yupo kwenye changamoto mpya.

Simba ipo mikononi mwa Charles Lukula raia wa Uganda ambapo hii itakuwa ni dabi yake ya kwanza ngoma itapigwa Uwanja wa Mkapa