REKODI NA KIKOSI CHA SIMBA V KAGERA SUGAR

KIKOSI cha Simba kitakachoanza dhidi ya Kagera Sugar, Uwanja wa Kaitaba hiki hapa:_

Manula ambaye hajafungwa kwenye mechi 10 akiwa ameyeyusha dakika 1306 leo ana kazi ya kuendelea kulinda rekodi yake.

Kapombe mchezo uliopita alitoa pasi moja ya bao

Zimbwe Jr ana pasi nne za mabao

Henock

Kaoute nyota pekee mwenye kadi nyekundu ndani ya Simba msimu huu

Chama alitoa pasi mbili na kufunga bao moja dhidi ya Geita Gold

Mzamiru alitoa pasi mchezo uliopita dhidi ya Geita

Bocco alitupia mechi iliyopita dhidi ya Geita Gold

Phiri kinara wa mabao ndani ya Simba akiwa nayo 10

Sakho alitupia mabao mawili mchezo uliopita