NYOTA YANGA WANAZIDI KUIMARIKA

UONGOZI wa Yanga umeweka wazi kuwa bado kasi ya wachezaji wa timu hiyo inazidi kuongezeka na watafanya vizuri mechi zao zijazo.

Kwenye mchezo wao uliopita dhidi ya Coastal Union miongoni mwa nyota ambao walipata nafasi ya kuonyesha uwezo wao ni pamoja na Fiston Mayele, Aziz KI, Feisal Salum, Gael na Aziz KI.

Ally Kamwe, Ofisa Habari wa Yanga amesema kuwa bado kasi ya wachezaji wa timu hiyo inaongezekana kutokana na maandalizi ambayo wanafanya.

“Unaona kwa sasa kila siku wachezaji wanazidi kuwa imara hili ni jambo la msingi na kila mmoja anapenda kuona hivi.

“Gael, Lomalisa, Aziz KI ni miongoni mwa wachezaji wazuri hapo sijawataka akina Feisal Salum, Kibwana hivyo kazi ipo na mashabiki wazidi kuwa pamoja nasi,”.

Mchezo ujao wa Yanga ni dhidi ya Azam FC unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa.