IKIWA ni kumbukizi yake leo Desemba 21 ya kuletwa duniani kiungo Pape Sakho kashuhudia timu yake ya Simba ikigawana pointi mojamoja na Kagera Sugar.
Moja ya mchezo uliokuwa ni wazi kwa timu zote mbili kusepa na pointi tatu muhimu lakini umakini wa safu za ushambuliaji kwa timu zote mbili ulikuwa ni hafifu.
Ni Deus Bukenya wa Kagera Sugar alianza kufunga dakika ya 15 kisha beki wa Simba Henock Inonga aliweka usawa dakika ya 38.
Pongezi kwa kipa wa Kagera Sugar, Said Kipao ambaye alikuwa imara kwenye lango lake kama ilivyokuwa kwa Aishi Manula ambaye amekwama kutookota nyavuni mpira.