BEKI wa Simba Henock Inonga amepachika bao lake la kwanza leo kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Kagera Sugar.
Ni dakika ya 38 Inonga alipachika bao hilo akiweka usawa ndani ya dakika 45.
Ni Kagera Sugar walianza kumtungua Aishi Manula kipa wa Simba ambaye hakuwa na chaguo kuokoa mpira huo.
Ilikuwa ni dakika ya 15 kupitia kwa Deus Bukenya ambaye aliwainua mashabiki wa Kagera Sugar.
Ni mchezo ambao una kasi kubwa kwa timu zote mbili zikiwa zinasaa pointi tatu muhimu