DESEMBA 21,2022 Ligi Kuu Tanzania Bara inatarajiwa kuendelea ikiwa ni mzunguko wa pili.
Tanzania Prisons wenye pointi 15 watawakaribisha Dodoma Jiji kutoka makao makuu wakiwa na pointi 18.
Pia Geita Gold wenye pointi zao 22 wao watamenyana na Azam FC wenye pointi 36.
Ngoma nyingine itakayopigwa ni Kagera Sugar yenye pointi 22 kibindoni dhidi ya Simba yenye pointi 37.
Kinara wa Ligi Kuu Bara ni Yanga akiwa na pointi zake kibindoni 44 baada ya kucheza mechi 17.