BENCHI la ufundi la Azam FC chini ya Kaimu Kocha Kali Ongala leo Desemba 21 limeshuhudia penalti iliyowaacha kwenye mshangao na kuwapa pointi moja mbele ya Geita Gold.
Dakika ya 68 mshambuliaji wa Geita Gold, Danny Lyanga alionekana akipambana kuingia kwenye 18 ya Azam FC na kugongana na mdogo wake Ayoub Lyanga.
Mwamuzi wa kati Omary Mode kutoka Tanga aliamuru iwe pig la penalti ambapo mpigaji Offen Chikola alimpoteza kipa namba mbili Wilbol Maseke dakika ya 69.
Bao hilo limesawazisha bao la Prince Dube ambaye alianza kuwatungua Geita Gold dakika ya 15 kipindi cha kwanza.
Baada ya penalti hiyo kutolewa wachezaji wa Azam FC walionekana wakilalamika lakini maamuzi ya mwamuzi hayakubadilika tuta likapigwa.
Azam FC wanafikisha pointi 37 baada ya kucheza mechi 17 za ligi msimu wa 2022/23.