YANGA YAIBAMIZA COASTAL UNION,DUA KWA NKANE

MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu Bara Yanga wameibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Coastal Union.

Mchezo wa ligi uliochezwa Uwanja wa Mkapa, dakika 90 Yanga ilikuwa kwenye umiliki wa mpira jambo lililoipa Coastal Union kutoboa ngome iliyokuwa chini ya nahodha Bakari Mwamnyeto.

Ni mabao ya Fiston Mayele ambaye ametupia mabao mawili na bao lingine moja ni mali ya Feisal Salum.

Bahati mbaya kwa kinda Dennis Nkane ambaye aliingia akitokea benchi alikwama kukamilisha dakika zilizobaki.

Nkane alipata maumivu dakika ya 80 na aliondolewa sehemu ya mchezo nafasi yake haikuchukuliwa na mchezaji kwa sababu Kocha Mkuu wa Yanga, Nasreddine Nabi alikuwa amekamilisha idadi inayotakiwa kufanyiwa mabadiliko.

Ugua pole Nkane ili urejee kwenye ubora wako