HELLO, MWENDELEZO WA MAYELE SOMO KWA WAZAWA

MWENDELEZO mzuri wa kucheka na nyavu upo kwenye miguu ya Fiston Mayele kinara wa utupiaji mabao ndani ya Ligi Kuu Bara akiwa ametupia mabao 11.

Alipowatungua Polisi Tanzania hakushangilia kwa mtindo wake wa kutetema bali alionekana kwa kitendo chake akipiga simu kisha akaongea na kuanza kushangilia.

Wanasema alikuwa anawapigiwa watani zake wa jadi pale Mwanza akimshtua mshakaji wake Moses Phiri kwamba ameshatupia kazi kwako huko.

Uzuri ni kwamba Mayele ukimuuliza kuhusu idadi ya mabao yake hajui kwa muda huo ila anachojua amefunga.

Kwenye upande wa ufungaji hapo kazi inazidi kuwa kwenye vita wageni wakitawala huku wazawa wakiwa kwenye mwendo wao.

Anayemfuatia Mayele ni Phiri wa Simba mwenye mabao 10 wazawa mwenye mabao mengi ni Sixtus Sabilo wa Mbeya City akiwa nayo saba kibindoni.

Wazawa wana kazi kubwa kwenye kuongeza juhudi kwenye kucheka na nyavu ili kuongeza ushindani kwenye nafasi ya ushambuliaji.

Nafasi ya walinda mlango angalau hii imekuwa ikiwatambulisha vema wazawa lakini eneo la ushambuliaji ni maji kupwa kujaa.

Mayele msimu uliopita alitupia mabao 16 tayari kafika nusu ya mabao yake akiwa ametupia 11 kabakiza mabao matano kuvunja rekodi yake.