HIZI HAPA ZA YANGA DESEMBA, NABI KUIBUKIA KWA MKAPA

BAADA ya kufungiwa mechi tatu kwa kosa la kumshambulia kwa maneno mwamuzi wa kati na wapembeni Kocha Mkuu wa Yanga, Nasreddine Nabi ataibukia kwenye Uwanja wa Mkapa mchezo dhidi ya Coastal Union.

Yanga ndani ya Desemba ina vigongo 7 ambapo Nabi kafungiwa kwenye mechi tatu kutokana na kosa hilo hicyo ni Cedric Kaze, kocha msaidizi wa Yanga atakuwa kwenye benchi la ufundi.

 Vigongo 7 kwa Yanga ndani ya dakika 630 ni mechi nne watakuwa nyumbani Uwanja wa Mkapa huku tatu wakiwa ugenini.

Kazi inatarajiwa kuanza Jumapili, Desemba 4 ambapo Yanga itamenyana na Tanzania Prisons, mchezo ujao itakuwa ni Namungo v Yanga, Desemba 7.

Yanga v Kurugenzi huu ni mchezo wa Kombe la Shirikisho raundi ya Pili unatarajiwa kuchezwa Desemba 9/11, Yanga v Polisi Tanzania, Desemba 17 kigongo kingine ni Yanga v Coastal Union, Desemba 20 hapa adhabu ya Nabi itakuwa imemeguka.

Vigogo hao watakutana na vigongo wenzao Azam FC  itakuwa Desemba 25 siku ya Sikukuu ya Christmas na kigongo cha mwisho itakuwa dhidi ya Mtibwa Sugar, Desemba 31 ambapo shughuli ya Desemba itafungiwa Uwanja wa Manungu, Morogoro.

Nabi hivi karibuni aliweka wazi kuwa ratiba ni ngumu kwao lakini wanapambana kutafuta matokeo chanya.

“Ukitazama ratiba kweli ni ngumu hilo lipo wazi na niliwaambia tangu mwanzo lakini sio sababu kwamba tukikosa matokeo iwe ni kigezo hapana, tunafanya maandalizi kutafuta ushindi kwa kila mechi,”.