HIVI HAPA VIGONGO VYA SIMBA DESEMBA

MWEZI wa shughuli huu hapa Desemba ambapo kila timu zina vigongo vya kazi kukamilisha mwaka 2022 na kuukaribisha 2023.

Simba nao wana kazi kubwa kusaka pointi tatu kwenye mechi ambazo wanacheza kusaka pointi tatu.

Kete za Simba ni 6 ambazo ni dakika 540 tayari wameshayeyusha 90 ndani ya uwanja.Vigongo viwili pekee watakuwa nyumbani na vigongo vinne ngoma itapigwa ugenini.

 Desemba 3,2022, Coastal Union 0-3 Simba, Uwanja wa Mkwakwani, Tanga hapo kete inayofuata ni Simba v Eagle kati ya Desemba 9/11 huu ni mchezo wa Kombe la Shirikisho raundi ya Pili.

Geita Gold v Simba, Desemba 18, Kagera Sugar v Simba, Desemba 21, KMC v Simba, Desemba 26 itakuwa ni siku ya Boxing Day, Simba v Tanzania Prisons, Desemba 30 kitakuwa kigongo cha mwisho kufunga mwaka 2022.

Mguda amesema kuwa hakuna namna ratiba imepangwa lazima ifuatwe.

“Ukizungumzia ugumu wa ratiba unaona, tunacheza nyumbani kisha tunasafiri kurudi kucheza, hamna namna ni ratiba imepangwa ni lazima tuifuate na kufanya maandalizi mazuri,”.