WAKATI Augustino Okra akirejea kikosi cha Simba anapishana na mwamba Gadiel Michael ambaye atakosekana kwenye mechi tatu za ushindani ndani ya Simba.
Okra alipata maumivu kwenye mchezo wa ligi uliopita dhidi ya Mbeya City na alikosekana kwenye mchezo dhidi ya Polisi Tanzania.
Kwa sasa yupo fiti na alikuwa sehemu ya wachezaji waliofanya mazoezi ya mwisho jana Desemba 2,2022 Uwanja wa Mkwakwani,Tanga.
Leo Simba ina kibarua cha kusaka pointi tatu mbele ya Coastal Union ambao nao wanazihitaji pia pointi tatu.
Beki Gadiel atakosekana kwenye mchezo huo kutokana na kufungiwa mechi tatu kwa kile ilichoelezwa kuwa alionekana akimwaga vitu vyenye unga katikati ya Uwanja wa Sokoine kwenye mchezo wa Mbeya City 1-1 Simba.
Ilikuwa ni Novemba 23,2022 Uwanja wa Sokoine,Mbeya na alianza kikosi cha kwanza kwenye mchezo dhidi ya Polisi Tanzania wakati ubao wa Uwanja wa Ushirika ukisoma Polisi Tanzania 1-3 Simba.