MESSI ALIKIWASHA LICHA YA KUKOSA PENALTI

GWIJI wa soka wa England na beki wa zamani wa Manchester United, Rio Ferdind amekiri kuwa nahodha wa Argentina, Lionel Messi alikuwa katika kiwango bora juzi Jumatano kwenye mchezo wa Kombe la Dunia.

Jumatano timu ya taifa ya Argentina ilishinda mabao 2-0 dhidi ya Poland katika mchezo wa Kombe la Dunia na kufuzu hatua ya 16 bora.

Messi ndani ya Argentina amefunga jumla ya mabao 93 hakuweza kufunga bao kwenye mchezo huo na alikosa penalti kipindi cha kwanza.

Nyota huyo mwenye miaka 35 anatajwa kuwa mwanasoka bora wa muda wote alifanikiwa kupiga pasi za uhakika kwenye mchezo huo wa kundi C.

Ferdinand alisema:”Ukweli ni kuwa hakuwa katika ubora kama wa zamani lakini alikuwa ni bora katika maeneo mengi dhidi ya Poland