KOCHA WA YANGA AFUNGIWA MECHI TATU KISA MANENO

Kocha wa klabu ya Young Africans SC, Nasreddine Nabi amefungiwa michezo mitatu na kutozwa faini ya Sh. 500,000 (laki tano) kwa kosa la kuwashambulia kwa maneno mwamuzi wa kati na mwamuzi wa akiba wa mchezo wa kipigo cha 2-1 cha klabu hiyo dhidi ya Ihefu FC.

Nabi aliendelea kufanya kitendo hicho hata baada ya kuonywa kwa kadi ya manjano.