>

DODOMA JIJI WAREJEA NYUMBANI

UONGOZI wa Dodoma Jiji umsema kuwa utaanza kutumia Uwanja wa Jamhuri, Dodoma kwenye mechi za nyumbani baada ya kufunguliwa.

Uwanja huo ulikuwa umefungiwa kwa matumizi kutokana na kutokidhidi vigezo hivyo kufunguliwa kwake ni baada ya vigezo kukamilika.

Ofisa Habari wa Dodoma Jiji, Moses Mpunga amesema kuwa wamepokea taarifa hizo kwa furaha na itakuwa ni mwanzo wao kuendeleza burudani nyumbani.

“Tumepokea barua ya kufunguliwa Uwanja wa Jamhuri hili ni jambo jema na zuri kwa kweli kikanuni Uwanja wa Liti ulikuwa wa nyumbani lakini ni kama tulikuwa ugenini vile.

“Disemba 12 tutaanza kuutumia uwanja huo ikiwa ni baada ya kukaguliwa mchezo wetu dhidi ya Ruvu Shoting Desemba 3 tutatumia Uwanja wa Liti.

“Mchezo wetu ujao utakuwa dhidi ya Coastal Union na tupo imara kwa kuwa kwenye mechi zetu dhidi ya Yanga na Namungo hatukuzalisha majeruhi hivyo mashabiki wajitokeze kwenye mchezo wetu ujao dhidi ya Coastal Union kuona tukichukua pointi tatu,”.